395px

Corona

Rayvanny

Corona, corona, corona
Corona, corona, corona

Wote tumuombe Mungu kwa hili janga
Ikibidi lipite
Tujihadhari na tujikinge
Ili lisitufike

Habari kote duniani zimesambaa
Ugonjwa unaua na hauna tiba
Na wengine wetu masikini hatujiwezi
Mwenyezi Mungu kawe tiba

Watoto wetu mashule, aah
Mama zetu tu sokoni
Kwenye vyombo vya usafiri makazini
Tujilinde

Osha mikono (aah)
Epuka mikusanyiko sio ya lazima (aah)
Na uonapo dalili
Mapema wahi hospitali

Corona, corona, corona
Corona, corona, corona
Corona, corona, corona
Corona, corona, corona

'Hatua zimeshaanza kuchukuliwa
Ameshatoa tahadhari mbalimbali
Ambazo tunatakiwa kuzichukua
Napenda nirudie ndugu zangu Watanzania
Kwamba ni vizuri sana tukaendelea kuchukua tahadhari, kwa nguvu zote
Ugonjwa huu unaua, na unaua kwa haraka sana
Niwaombe ndugu zangu Watanzania
Tusipuuze ungonjwa huu
Tusipuuze hata kidogo
Ni lazima tuanze kuchukua hatua
Za kujikinga kwa tatizo hili

Corona, corona, corona
Corona, corona, corona
Corona, corona, corona
Corona, corona, corona

Escrita por: