Letra

    Ah, barua yako uliyotuma kwa Ricardo Momo nimeisoma
    Ila nimechelewa kuijibu sababu moyoni imenchoma
    Eeh, nliyo yategemea tofauti na nlicho kiona
    Hata naandika hii barua huku roho yangu inansonona

    Umesema nichane nguo pia funguo
    Umeirudisha sawa
    Simu niziweke kituo na sio chaguo
    Nikome kabisa sawa
    Umesema hata ile picha nzuri
    Nliyo kukumbatia niichane sawa
    Ila kinachoniumiza
    Mbona moja umesahau

    Kosa langu kosa langu
    Hujaniambia
    Na kuniacha peke yangu
    Ukanikimbia
    Ila mbona kosa langu
    Hujaniambia
    Nami nikabiki peke yangu
    Ukanikimbia

    Aah
    Mbona ukanichimbia kaburi ningari bado mzima
    Niife nizikwe vizuri nipotee kabisa kimya
    Licha ya matendo mazuri kwa upendo na heshima
    Moto ukachochea tanuri ukachoma wangu mtimaa

    Natamani hata ningepata nafasi
    Muda wakati kukutazama
    Unione hata japo sura
    Unitazame macho yangu
    Mwenzako wimbi limenipiga kasi
    Langu jahazi limezama
    Mnyonge mwana sanura
    Wee ndio ulikuwa furaha yangu

    Tatizo hata nkilia wa kunifuta machozi sina
    Sawa na gari lisio na gear
    La kuiforce ipande mlima
    Ndio maana siishi kulalama
    Japo jibu moja tuu
    Linaloniumiza
    Mwenzio bado sijaelewa

    Kosa langu kosa langu (kosa langu)
    Hujaniambia (hujaniambia)
    Na kuniacha peke yangu (peke yangu)
    Ukanikimbia (ukaenda)
    Ila mbona kosa langu (kosa langu)
    Hujaniambia (hujaniambia bado)
    Nami nikabi peke yangu (peke yangu)
    Ukanikimbia (ukaenda ooh)

    (Oh moyo)
    Moyo wangu umevunjika una magongo
    (Oh moyo)
    Kila sehemu nayoshika kinyamazongo
    (Oh moyo)
    Hata chozi likifutika linabaki tongo
    (Oh moyo)
    Najitahidi kulidhika ila nna kinyongo

    (Oh moyo)
    Moyo wangu umevunjika unaa jamani
    (Oh moyo)
    Hhhmm hum


    Comentarios

    Envía preguntas, explicaciones y curiosidades sobre la letra

    0 / 500

    Forma parte  de esta comunidad 

    Haz preguntas sobre idiomas, interactúa con más fans de Diamond Platnumz y explora más allá de las letras.

    Conoce a Letras Academy

    ¿Enviar a la central de preguntas?

    Tus preguntas podrán ser contestadas por profesores y alumnos de la plataforma.

    Comprende mejor con esta clase:

    0 / 500

    Opciones de selección