visualizaciones de letras 7
Letra

    Pole pole pole pole
    Pole pole moyo wangu
    Masikini pole
    Pole mtima wangu

    Haikuwa dhamira
    Haikuwa kusudi langu
    Haikuwa dhumuni waala
    Haikuwa malengo yangu
    Ila tuseme labda moyo
    Pengine sio ridhiki
    Maana nimejitahidi sana
    Malengo hayafiki

    Kama kuswali naswali sana
    Mpaka sunna za usiku
    Kazi nimetafuta saana
    Ila siambulii kitu
    Sitaki kukufuru mungu
    Sababu najua ni mapito
    Japo inakatisha tamaa
    Ila siku yangu ipoo moyo

    Usiumiee (moyo wangu)
    Ni mapito (ooh moyo)
    Haya yote mitihani na yana mwisho
    Moyo wangu moyo
    Usiumie (moyo)
    Ni mapito (ooh moyo)
    Haya yote mitihani na yana mwisho

    Penzi maua
    Pesa mbolea
    Hata shemeji yako Ana
    Mengi ila hawezi ongea

    Moyo
    Najitahidi jiepusha vya watu ni majaribu aah
    Japo nna shida ila naepuka tamaa
    Moyo nlitamani siku moja na mimi nimjengee mama
    Ila ndo vile tu umasikini, mipango inakwama
    Hua naumia watoto shuleni wakifukuzwa ada
    Najiona mjinga yani sio bora baba
    Sitaki kukufuru mungu, najua ni mapito
    Maana riziki mafungu, nami langu siku lipo
    Moyo

    Usiumie (moyo wangu)
    Ni mapito (ooh moyo)
    Haya yote mitihani na yana mwisho
    (Moyo wangu moyo)
    Usiumie (jikaze moyoo)
    Ni mapito (ooh moyo)
    Haya yote mitihani na yana mwisho
    Moyo ooh
    Moyo ooh, ooh


    Comentarios

    Envía preguntas, explicaciones y curiosidades sobre la letra

    0 / 500

    Forma parte  de esta comunidad 

    Haz preguntas sobre idiomas, interactúa con más fans de Diamond Platnumz y explora más allá de las letras.

    Conoce a Letras Academy

    ¿Enviar a la central de preguntas?

    Tus preguntas podrán ser contestadas por profesores y alumnos de la plataforma.

    Comprende mejor con esta clase:

    0 / 500

    Opciones de selección