
Dunia
Harmonize
Mmh mmh
Nikifikiria dunia uwaga sipati jibu
Nawaza mpaka nadata
Nikikuuliza nini dunia
Huwezi kunipa jibu hapo ndo napata utata
Mmh
Muda mwingine unaweza dhani ni utani
Mbona vitu vizuri vyote viwe ni vya shetani
Eti muziki shetani
Pesa nazo shetani
Mpira na pombe shetani
Ngono na mihadarati shetani
Naamini Mungu yupo najua
Ndo ananifanya ninapumua
Akitaka hata sasa atanichukua
Ila mimi nataka kujua
Ni nini dunia
Dunia dunia
Hivi ni nini dunia
Dunia eeh
Mmh
Wanaoishi kwa imani
Misikitini makanisani
Uwepo wao hauonekani
Hali zao zipo taabani
Hivi ulikuaga wapi before
Haujaja duniani
Na kwanini kunakifo
Unapokwenda hapajulikani
Sawa safari ni yetu sote
Na hakuna aliyekwenda na akarudi
Japo kutusimulia
Kama pazuri ama pabaya
Uwe tajiri ama masikini
Kwa mchanga utarudi
Ninacho wahusia
Tusiishi kwa ubaya
Kuna kidude kinaitwa mapenzi
Hakijawahi kueleweka
Wakati wewe unalia
Mwenzako huku anacheka
Hivi ni nini dunia
Dunia dunia
Ni nini dunia
Dunia eeh
Muheshimiwa Kassim Majaliwa
Msalimie CDF Manete
Wapi IGP kamanda siro
Tuombeane mwisho mwema (eeh eeh yeah)
Tuombeane mwisho mwema (maana hakuna anaejua kesho)
Tuombeane mwisho mwema (kama wewe
Ni muislamu omba kwa Diniz yako)
Tuombeane mwisho mwema (kama wewe no mkristo omba kwa dini yako)
Tuombeane mwisho mwema (hakuna anaejua kesho no Siri no siri)
Tuombeane mwisho mwema (nisiri nisiri)
Tuombeane mwisho mwema (tuombeane nisiri)
Eyoo Kenny
Ni Siri no sirii eeh
Ni nini dunia
Dunia dunia
Hivi ni nini dunia hii



Comentarios
Envía preguntas, explicaciones y curiosidades sobre la letra
Forma parte de esta comunidad
Haz preguntas sobre idiomas, interactúa con más fans de Harmonize y explora más allá de las letras.
Conoce a Letras AcademyRevisa nuestra guía de uso para hacer comentarios.
¿Enviar a la central de preguntas?
Tus preguntas podrán ser contestadas por profesores y alumnos de la plataforma.
Comprende mejor con esta clase: