visualizaciones de letras 1

Nitafika Tu (feat. Bahati Bukuku)

Maggie Muliri

Letra

    Nina imani nitafika
    Jibu ni kufika
    Japo uwoga na wasi wasi
    Nitafika niendapo

    Jibu kwa moyo mwangu, nitafika eeeh
    Natamani kuenda kule nionapo
    Nina shauku ya kutekeleza
    Maono yangu eeh

    Lakini vikwazo ni vingi sana
    Lakini majaribu ni mengi sana
    Oooh wa kunivunja moyo
    Ni wengi sana njiani

    Pharao na jeshi lake hawataki kuniacha
    Jibu kwa moyo wao, nitafika
    Japo milima na mabonde
    Nitafika nitafika niendapo ooh

    Nahitaji nehema yako Jehovah
    Nifike niendapo ooh
    Nahitaji msaada wako baba
    Nifike niendapo ooh

    Naomba nishike mkono
    Nifike niendapo
    Jibu kwa moyo wangu
    Nikufika

    Bado nina pumzi, tumaini langu lipo (nitafika tu)
    Sikupata leo, kesho inakuja oooh (nitafika tu)
    Baada ya kesho, mwezi ujao unakuja (nitafika tu)
    Najipa moyo mwaka kesho nitafaulu eeh (nitafika tu)

    Hata kama jaribu lako lilikuwa ngumu wewe (utafika tu)
    Huruma ya Mungu imekutafuta leo (utafika tu)
    Hata kama mapito yalikuwa ni mengi kwako (utafika tu)
    Wema wa Mungu umekutafuta leo (utafika tu)

    Nikufika nikufika wee (utafika tu)
    Nikufika nikufika wee (utafika tu)

    Ata usiku uwe mrefu kutakucha
    Ata giza iwe kubwa nuru itatokea
    Jibu ya maisha yako ipo leo

    Ata safari iwe na vikwazo utafika
    Hata jaribu liwe nzito utavuka
    Jibu ya maisha yako ipo leo

    Unamkumbuka Sara alipata mtoto uzeeni
    Unamkumbuka Hannah mpaka alichekwa oooh
    Kumbe tumboni mwake amembeba Samweli
    Nehema ya Mungu bado iko nawe

    Yamkini huduma yako imebeba vitu vingi
    Hata giza liwe kubwa nuru nayo ipo
    Nehema ya Mungu bado iko nawe

    Hata maji yawe marefu basi kuna ukingo wake
    Nehema ya Mungu bado iko nawe
    Huruma ya Mungu bado inakutafuta aah

    Nimejitahidi sana bila mafanikio (nitafika tu)
    Haijalishi shida, vikwazo safarini wee (nitafika tu)
    Sijali wangapi wananikatisha tamaa (nitafika tu)
    Wala sitajali mazingira ninayoyapitia (nitafika tu)

    Hata kama jaribu lako lilikuwa ngumu wewe (utafika tu)
    Huruma ya Mungu imekutafuta leo (utafika tu)
    Hata kama mapito yalikuwa ni mengi kwako (utafika tu)
    Wema wa Mungu umekutafuta leo (utafika tu)

    Nikufika nikufika wee (utafika tu)
    Nikufika nikufika wee (utafika tu)


    Comentarios

    Envía preguntas, explicaciones y curiosidades sobre la letra

    0 / 500

    Forma parte  de esta comunidad 

    Haz preguntas sobre idiomas, interactúa con más fans de Maggie Muliri y explora más allá de las letras.

    Conoce a Letras Academy

    ¿Enviar a la central de preguntas?

    Tus preguntas podrán ser contestadas por profesores y alumnos de la plataforma.

    Comprende mejor con esta clase:

    0 / 500

    Opciones de selección