visualizaciones de letras 4

Binti Kiziwi

Z Anto

Letra

    Nimpate vipi mi sijui
    Nina imani mapenzi hayajui
    Nitapata ugonjwa wa moyo
    Kwa sababu ya mawazo
    Ninavyo jua maisha yake
    Hajawahi kuwa na boyfriend
    Ila ni mimi wa kwanza
    Na ninashindwa kumpata

    Kwa ishara naonekana nampenda
    Yeye eti mi namzingua
    Eti kama angilikua anasikia
    Basi ukweli wangu angeujua
    Kwa ishara naoneka nampenda
    Yeye eti mi namzingua
    Eti kama angelikua anasikia
    Basi ukweli wangu angeujua

    Ningemzowea rafiki yake
    Basi mi ningemtuma
    Ningezitambua ishara zake
    Kwake mi ningefika
    Ningemzowea rafiki yake
    Basi ningemtuma
    Ningezitambua ishara zake
    Kwake mi ningefika

    Sicilia ninampenda
    (Binti kiziwi)
    Moyo wangu wamtaka
    (Binti kiziwi)
    Sicilia nateseka juu yake
    (Yeye binti Kiziwi)
    Sicilia ninampenda
    (Binti kiziwi)
    Moyo wangu wamtaka
    (Binti kiziwi)
    Kichwa kinauma mawazo
    (Kwake binti kiziwi)

    Nashangaa pale napomkuta
    Akiwa na wenzake wanaongea
    Huwa najiuliza mimi
    Wanaongea naye vipi
    Nashangaa pale napomuita
    Nahisi huwa anakataa

    Sijui ndio hasikii
    Au mapozi au mapozi naye
    Afadhari angejua kusoma
    Hata hatari ujumbe ningempa
    Eti kama ningejua ishara
    Basi kwake ningefika mimi
    Afadhari angejua kusoma
    Hata bonge ujumbe ningempa
    Eti kama ningejua inshara
    Basi kwake ningefika baby

    Sicilia ninampenda
    (Binti kiziwi)
    Moyo wangu wamtaka
    (Binti kiziwi)
    Nateseka juu yake
    (Yeye binti Kiziwi)
    Sicilia ninampenda
    (Binti kiziwi)
    Moyo wangu wamtaka
    (Binti kiziwi)
    Kichwa kinauma mawazo
    (Kwake binti kiziwi)

    Binti kiziwi yuko full
    Yani yuko bomba
    Amenidatisha mnyamwezi na yake figa
    Tatizo moja tu ambalo mimi linanisibu
    Kila kukicha hata nikiwaza mi sipati jibu
    Nikimuambia neno I love you
    (Wala halijui)
    Nikimuambia neno I need you
    (Halitambui)
    Nikimuimbia nyimbo nzuri hata haisikii
    Pingu nasikitika nikimuona binti kiziwi
    Nikimuambia neno I love you
    (Wala halijui)
    Nikimuambia neno I need you
    (Halitambui)
    Nikimuambia nyimbo nzuri hata hasikii
    Pingu nasikitika nikimuona binti kiziwi
    Hata kusema neno I love you
    Kwake halijui
    Hata kusema neno I need you
    Kwake halitambui
    Hata kusema neno I love you
    Kwake halijui
    Hata kusema neno I need you
    Kwake halitambui
    Baby, baby baby, baby boo
    Baby I love you
    Ingawa nateseka tu naye
    Baby I need you
    Baby, baby boo
    Baby I love you
    Baby tu baby I need you

    Sicilia ninampenda
    (Binti kiziwi)
    Moyo wangu wamtaka
    (Binti kiziwi)
    Sicilia nateseka juu yake
    (Yeye binti Kiziwi)
    Sicilia ninampenda
    (Binti kiziwi)
    Moyo wangu wamtaka
    (Binti kiziwi)
    Kichwa kinauma mawazo
    (Kwake binti kiziwi)
    Sicilia ninampenda
    (Binti kiziwi)
    Moyo wangu wamtaka
    (Binti kiziwi)
    Sicilia nateseka juu yake
    (Yeye binti Kiziwi)
    Sicilia ninampenda
    (Binti kiziwi)
    Moyo wangu wamtaka
    (Binti kiziwi)
    Kichwa kinauma mawazo
    (Kwake binti kiziwi)


    Comentarios

    Envía preguntas, explicaciones y curiosidades sobre la letra

    0 / 500

    Forma parte  de esta comunidad 

    Haz preguntas sobre idiomas, interactúa con más fans de Z Anto y explora más allá de las letras.

    Conoce a Letras Academy

    ¿Enviar a la central de preguntas?

    Tus preguntas podrán ser contestadas por profesores y alumnos de la plataforma.

    Comprende mejor con esta clase:

    0 / 500

    Opciones de selección