Nafasi/Nishapona

Harmonize

Letra

    Imani nafsi inaniambia
    Haukuwa fungu langu
    Na sidhani kama nilikosea
    Kuukabidhi moyo wangu

    Ulinidanganya mapenzi ni zuri basi
    Panda twende safari
    Bila kujua la kwako ni mwendo kasi
    Ghafla ukanipa ajali

    Upweke umetawala nafsi
    Mwenzako usiku silali
    Ninahesabu mabati
    Kisa wewe

    Sijutii moyo wangu
    Kupenda nisipopendwa
    Sirudii makosa yangu
    Ujinga wakati wakwenda

    Kinachoniuma roho yangu ooh
    Kuwapa neno wahenga
    Maana si kwa posti zangu
    Na kujinadi napendwa

    Nishapona, nishapona
    Nishapona ila mazoea
    Basi nenda umwambie

    Nishapona
    Ooh mwambie
    Basi umwambie eeh
    Nishapona ila mazoea

    Heshima kunyenyekea
    Nilivyomnyenyekea
    Akaniona si chochote kwake
    Mazima akanipotezea
    Akanipotezea, alipomaliza shida zake

    Na bado siamini kweli ndo yule
    Alokuwa akisema, halali asiponiona
    Na kujilisha ya nini? Yote ni bure
    Nikamwita chanda chema, alinidanganya

    Zile miziki za kunichombeza, zinaniuma roho
    Mara akinidekeza, elaji njoo
    Ungesema nilipoteleza, nikamwomba koo
    Si vyema amenitelekeza mb kisadoo

    Basi nenda umwambie, nishapona
    Ooh mwambie
    Basi umwambie eeh
    Nishapona ila mazoea

    Basi nenda umwambie, Nishapona
    Ooh mwambie
    Basi umwambie eeh
    Nishapona ila mazoea

    Nenda kamwambie naja
    Nenda kamwambie naja
    Basi nenda kamwambie naja
    Nenda kamwambie naja


    Comentarios

    Envía preguntas, explicaciones y curiosidades sobre la letra

    0 / 500

    Forma parte  de esta comunidad 

    Haz preguntas sobre idiomas, interactúa con más fans de Harmonize y explora más allá de las letras.

    Conoce a Letras Academy

    ¿Enviar a la central de preguntas?

    Tus preguntas podrán ser contestadas por profesores y alumnos de la plataforma.

    Comprende mejor con esta clase:

    0 / 500

    Opciones de selección