Suscríbete

Kitoroli (feat. Domo Kaya)

Malkia Karen

Letra

    Umeniburuza ka kitoroli
    Kutwa kunipeleka puta
    Ile sandaka lawe
    Ukaniona mpori pori
    Kukupenda ukavimba kichwa
    Leo bora ninawe

    Sikudhani siku moja
    Kama nitakuja toa machozi
    Kwa ajili yako na nilalame iyeee
    Kukuganda ka ruba
    Kuonyesha upendo hukujali
    Kabisa maa ee, ooh maa eeh

    Natembelea magongo (aah)
    Mzima bado nachechema (aah)
    Ila kwa hali sio shwari
    Nisije nikatoka chongo
    Kwa mapenzi kung'ang'ana
    Nikadhoofu hali

    Nalia mwenyewe, mwenyewe
    Japo nina ugonjwa moyoni sijui lini nitapona
    Nalia mwenyewe
    Mgonjwa nakatisha dozi bora nitoweke duniani
    Nalia mwenyewe, mwenyewe
    Mgema kasifiwa pombe kaitia maji nanyotokwa
    Nalia mwenyewe, nitazoea hali yangu

    Don't cry baby, we unadhani itakuaje
    Ukiondoka ukasepa na moyo wangu mfa maji
    Don't cry baby, we unadhani itakuaje
    Ukiondoka ukasepa na moyo wangu mfa maji
    Si unataka kunitosa
    Na unajua mapenzi hayana kocha (kweli nimekubali)
    Najua umechoka
    For the first time natambua makosa (kweli nimekubali)
    Mwisho wa wiki hazikuniisha safari
    Vishawishi kasababisha dosari
    Najikuta nagonganisha magari
    Ooh mama ma

    Hapo sasa umenishika sharubu
    Tungi tungi nyumbani unafanya kusudi kunisulubu
    Tumpe faida nani?
    Mdomo juu juu unataka niwe bubu
    Siwezi kukuchapa makofi utakuwa sugu
    Kwanza mapenzi matamu kati ni msala
    Unapopungua upendo na kugeuka biashara
    Kosa pesa ulale kwenye kochi
    Kodoa macho tochi

    Nalia mwenyewe, mwenyewe
    Japo nina ugonjwa moyoni sijui lini nitapona
    Nalia mwenyewe
    Mgonjwa nakatisha dozi bora nitoweke duniani
    Nalia mwenyewe, mwenyewe
    Mgema kasifiwa pombe kaitia maji nanyotokwa
    Nalia mwenyewe, nitazoea hali yangu


    Comentarios

    Envía preguntas, explicaciones y curiosidades sobre la letra

    0 / 500

    Forma parte  de esta comunidad 

    Haz preguntas sobre idiomas, interactúa con más fans de Malkia Karen y explora más allá de las letras.

    Conoce a Letras Academy

    ¿Enviar a la central de preguntas?

    Tus preguntas podrán ser contestadas por profesores y alumnos de la plataforma.

    Comprende mejor con esta clase:

    0 / 500

    Opciones de selección